Idadi ya Wagonjwa wa Dengue yapaa, 3 Wafariki Dunia Dar es Salaam


Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema idadi ya wagonjwa waliothibitika kuwa na homa ya dengue imeongezeka kwa kasi hadi kufikia Juni Mosi imefika 3,495 kutoka 2,971 idadi ya kuanzia januari 1 hadi Mei 29, 2019.

Ambapo takwimu hizo, kati ya wagonjwa 3,333 na vifo vya watu 3 vimetokea mkoa wa Dar es salaam.

“Kati ya watu waliopimwa waliogundulika kuwa na virusi au walikwishapata homa ya dengue 3,333 ni kutoka Dar es Salaam, 135 jijini Tanga, 19 kutoka Pwani, 6 Morogoro, Singida mmoja na Kilimanjaro pia mmoja.”

“Takwimu za ugonjwa huu kutoka Januari hadi Juni 2019 ni kama ifuatavyo, Januari kulikuwa na wagonjwa 56, Februari 82, Machi 159, Aprili 678 na vifo viwili, Mei 2,485 na kifo kimoja,” amesema Ummy Mwalimu.


Kufuatia hali hiyo Waziri Ummy ameagiza kila nyumba na mtaa kuhakikisha maofisa afya wa wanafuatilia upuliziaji dawa hizo, huku akitoa angalizo la kuwepo kwa dawa feki ambazo hazisaidii kuangamiza mazalia hayo, hivyo akaelekeza wapuliziaji wahakikiwe ili mwananchi ajue wanaotambulika na manispaa husika.

“Lazima tuweke mazingira yetu safi na salama, niseme tu ugonjwa wa homa ya dengue si mpya na unaathiri nchi nyingi, jumla ya watu milioni 390 huugua ugonjwa huu nchini na vifo ni 40,000 pekee, lakini Malaria watu milioni 216 wanaugua kila mwaka ila vifo ni 450,000 hivyo bado malaria ni tishio,” amesema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad