Dar es Salaam , Tanzania : Ukiwa ni mji mkubwa zaidi na wenye wingi wa watu kwa Tanzania, huku baadhi ya watu kama utawauliza wanadiriki kusema hakuna Tanzania bila Dar es Salaam, kwani ndipo pahala ambapo kuna kila kitu, kuanzia starehe hadi tamaduni za watu tofauti tofauti na ndiyo kiini cha uchumi wa Nchi. Ni Ukweli kuwa Dar es Salaam ni jiji linalokua kwa kasi sana. Leo tunaomba tujuzane juu ya miji mitano mikubwa zaidi barani Afrika huku Dar Es Salaam ya wazaramo ikiwa haijafua dafu.
1. Lagos, Nigeria:
Ikiwa na wakaazi 16,060,303 Lagos inafanikiwa kuwa jiji kubwa Afrika, kwa kuwa na kiwango kikubwa cha kipato kwa mtu mmoja mmoja GDP, na kulifanya kuwa jiji tajiri na kituo cha uchumi nchini Nigeria. Cha ajabu zaidi ni kuwa biashara kubwa zaidi katika jiji hili ni biashara ya usafirishaji kupitia mabasi, na kulifanya kuwa maarufu zaidi Afrika.
2. Cairo, Egypt :
Wakazi takribani milioni 20,230,350 Cairo linaweza kuwa jiji muhimu zaidi Barani Afrika kwa kuwepo kwa historia kubwa na ugunduzi mbalimbali. Kama Piramidi zilizopo. Sio tu ni jiji la pili kwa ukubwa bali ni jiji lenye mchanganyiko wa watu wengi kwa Afrika ya Kati, na la 15 kwa ukubwa duniani. Ukiwa Cairo sio tu kwamba utatembelea Maeneo ya utalii, bali ndio jiji ambalo hali lali Watu wake wanapilika pilika masaa 24. Na kulifanya kuwa miongoni mwa majiji machache sana duniani ambayo unaweza kupata huduma yoyote kwa muda wowote.
3. Kinshasa, Democratic Republic of Congo:
Watu 10,130,000 jijini Kinshasa, na uliweka pamoja na mji wa Brazzaville, jiji lililopo karibu na mto Congo. Brazzaville ni mji mkuu wa Jamhuri ya Congo kukiwa na watu milioni 1.37. huku Kinshasa kukuwa na wakazi zaidi ya milioni 10 million, hivyo jumla kukiwa na watu takribani milioni 12.
4. Abidjan, Ivory Coast:
Wakazi zaidi ya 4,765,000 na kulifanya jiji hili kuwa na asilimia 20 ya wakazi wote wa nchini Ivory Coast. Jiji ambalo mwaka 1931 lilitanuliwa, na sababu nchi ya Ivory coast ilitawaliwa na Ufaransa, asilimia kubwa lugha inayotumia hapa ni Kifaransa. Kituo kikuu cha watalii nchini humo.
5. Johannesburg, South Africa:
Kukiwa na watu zaidi ya 4,434,827 ni mji mkubwa zaidi Nchini South Afrika, pia ni miongoni sehemu 50 za miji duniani ambazo ni kubwa, japo kuwa sio mji mkuu wa South Africa. Ni jimbo tajiri sana la Gauteng. Biashara ya madini kwenye kilima cha Witwatersrand kimechangia ukuaji wa mji huu, pamoja na kua kituo kikubwa cha biashara, utalii, ambapo pia kuna hifadhi za wanyama ya Johannesburg na Krugersdorp hifadhi ya asili.