Wapelelezi kutoka taasisi ya kupambana na ugaidi nchini India wamemkamata mtu mmoja anayeshukiwa kuwa na uhusiano na mtu aliyejitoa muhanga wakati wa matukio ya mashambulizi ya siku ya Pasaka nchini Sri Lanka.
Maafisa wa upelelezi wamesema Mohammad Azharuddin, 32, alikua rafiki na Zahran Hashim kwenye mtandao wa Facebook, mtu anayedaiwa kuwa mpangaji wa mashambulizi, kama ilivyodawaiwa na wanamgambo wa Islamic State (IS).
Kukamatwa huko kulikuja baada ya kuvamia mahabusu inayoshukiwa kuwa ya wanamgambo wa IS katika mji wa kusini mwa India, Coimbatore.
Mashambulizi ya mabomu talisababisha vifo vya zaidi ya watu 250 na kuwajeruhi 500 wengine .
Kwa Picha: Shambulio la makanisa Sri Lanka
Kundi la kiislamu la Thowheed Jamaath ladaiwa kuhusika na mashambulizi ya makanisa
Watu wengine watano wamekamatwa kwa ajili ya mahojiano, limeeleza shirika la upelelezi la India (NIA), ambao walivamia eneo hilo na kuwakamata.
Ilifungua kesi dhidi ya Bwana Azharuddin na wengine tarehe 30 mwezi Mei, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari.
Maafisa wa intelijensia na polisi wanaendelea na msako hasa katika mji wa Ukkadam, jirani na mji wa Coimbatore, ambapo maafisa wanasema washukiwa watatu, akiwemo Azharuddin, wanaishi.
Hakimiliki ya Picha @NIA_India@NIA_INDIA
Mamlaka nchini humo zinawashutumu washukiwa sita kwa kupandikiza propaganda za IS na kujaribu kuwavuta ''vijana '' kutekeleza mashambulizi kusini mwa India, ikiwemo jimbo la Tamil Nadu, jimbo ambalo mji wa Coimbatore unapatikana.
Image caption
Zahran Hashim anadaiwa kuwa kiongozi wa waliotekeleza mashambulizi ya mabomu
Mamlaka nchini Sri Lanka zimekana ripoti kuwa zimeshindwa kufanyia kazi tahadhari zilizotolewa Marekani na idara ya intelijensia ya india kuhusu kuwepo kwa tishio la mashambulizi.
Taasisi ya NIA imekuwa na mfululizo wa msako kusini mwa India tangu mwezi Aprili .
Mwezi Aprili mtu mmoja alikamatwa katika jimbo la Kerala ambaye alikua anashutumiwa kupanga shambulio la kujitoa muhanga.
Watu kadhaa pia wanaoshukiwa kuwa na mahusiano na wanamgambo wa IS walishutumiwa kupanga mashambulizi mjini Delhi, shirika la habari la Uingereza, Reuters limeripoti.
India Yamkamata mtu Anayeshukiwa Kutekeleza Mashambulizi katika Kanisa Sri Lanka
0
June 13, 2019
Tags