Iran yatangaza itakiuka makubaliano ya nyuklia na kuongeza urutubishaji wa Uranium

Iran imetangaza kwamba itakiuka kiwango cha urutibishaji wa madini ya Uranium Juni 27, kilichowekwa katika makubaliano ya nyuklia ya mnamo 2015 yalioidhinishwa na mataifa yenye nguvu duniani.

Shirika la nishati ya atomiki nchini Iran limesema limeongeza mara nne uzalishaji wa madini hayo yanayotumika kutengeneza nishati lakini pia silaha.

Lakini limeongeza kwamba bado "kuna muda" kwa mataifa ya Ulaya kuwajibika kwa kuilinda Iran dhidi ya vikwazo vilivyoidhinishwa upya vya Marekani.

Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimeionya Iran dhidi ya hatua hiyo inayokwenda kinyume na makubaliano hayo.


Zimesema hazitokuwa na namna ila kuidhinishia upya vikwazo, ambavyo zilikubali awali kuviondoa iwapo Iran itatii masharti yaliowekwa katika mpango wake wa nyuklia.

Iran imelalamika kwamba mataifa hayo yameshindwa kutii uwajibikaji wao katika kutatua athari za vikwazo vya Marekani vilivyoidhinishwa baada ya rais Donald Trump kujito akatika mpango huo mwaka jana.

Trump anataka kuilazimisha Iran kujadili upya makubaliano hayo na ikubali kusitisha mpango wake wa nyuklia na isitishe shughuli zake katika enoe la mashariki ya kati.

Hatua hii ya sasa inajiri wakati ambapo kuna wasiwasi mkubwa katika eneo, huku Marekani ikituma jeshi na kuishutumu Iran kwa kuhusika katika mashambulio yanayoshukiwa yaliosababisha magari mawili ya mafuta kuteketea moto siku ya Alhamisi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad