MBUNGE wa Jimbo la Starehe, Charles Njagua (Jaguar), ataendelea kubaki mahabusu kwa siku tano katika kituo cha polisi cha Kileleshwa wakati uchunguzi kuhusu kesi yake ya uchochezi ikiendelea.
Uamuzi huo unatokana na upande wa mashtaka kutoa siku tatu za kikazi za kufanya uchunguzi huo, bila kuzijumuisha Jumamosi na Jumapili, wiki hii.
Awali, upande wa mashitaka ulitaka Jaguar abaki mahabusu kwa siku 14 katika kituo cha polisi cha Kamukunji ili kukamilisha upelelezi huo.
Jaguar aliyekuwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Sinkyani Tobiko, anakabiliwa na mashtaka ya kutoa kauli ya uchochezi dhidi ya wafanyabiashara wa kigeni nchini humo jijini Nairobi katika Barabara ya Kirinyaga alipowataka wafanyabiashara hao kuondoka nchini humo la sivyo watashambuliwa.