Kapombe Aumia Tena Kwenye Mazoezini

BEKI wa klabu ya Simba na Taifa Stars, Shomary Kapombe ameumia tena kwenye mazoezi ya timu ya Taifa ambayo yalikuwa yanafanyika uwanja wa Taifa.



Kapombe ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa majeraha ambayo aliyapata mwisho wa mwaka jana kwenye kambi ya timu ya taifa akijiandaa na mechi dhidi ya Lesotho.

Kapombe amejitonesha kwenye mazoezi maalumu aliyokuwa akifanya chini ya uangalizi wa madaktari wa timu ya Simba na Taifa Stars na anaweza kukosekana kwenye msafara wa wachezaji wa Tanzania ambao June 07, wataelekea nchini Misri kwa ajili ya kuweka kambi ya maandalizi ya Fainali za mataifa Afrika (Afcon 2019).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad