Kauli ya Rais Magufuli 'kuwaacha Mabilionea 100' yamuibua Zitto, Lema


Jana Rais John Magufuli aliyoitoa kauli ya kwamba anatamani atakapomaliza muda wake wa uongozi aache mabilionea 100 nchini Tanzania. Kauli ambayo imewaimbua wanasiasa wawili nchini Tanzania.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka Wilaya zote nchini kwenye mkutano wa siku nzima uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali.

Kauli hiyo ya Magufuli imeonekana kuwakuna baadhi ya wanasiasa, akiwemo mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe na mwenzake wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ambao walitumia mtandao wa kijamii wa Twitter kueleza  hisia zao kutokana na kauli hiyo ya Magufuli.

Lema alieleza kuwa hotuba ya Rais Magufuli katika mkutano huo imejaa matumaini hasa kwa kauli yake ya kuacha mabilionea 100.

“Kauli ya Rais kuwa anataka kuona Tanzania ya mabilionea100 kabla ya kumaliza muda wake wa uongozi ni kauli ya matumaini kwa nchi.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad