Kauli ya Serikali Kuhusu Watumishi wa Umma Wanaojifungua Mapacha au Watoto Njiti

Serikali  imesema kanuni za kudumu za utumishi wa umma za mwaka 2009 hazijaanisha masharti ya likizo ya uzazi kwa wanawake wanaojifungua mapacha zaidi ya wawili au watoto njiti.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Juni 25, 2019 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Mary Mwanjelwa wakati akijibu swali la mbunge wa Viti maalum (Chadema), Anatropia Theonest.

Anatropia amehoji ni muda gani wamekuwa wakipewa wazazi (mtumishi mwanamke au mwanaume) pale wanapopata watoto mapacha zaidi ya wawili au watoto njiti.

“Ikitokea mtumishi wa umma kajifungua watoto mapacha zaidi ya wawili au watoto njiti na kulazimika kuwa na muda zaidi wa kuhudumia watoto hao, mwajiri wake anapaswa kuwasilisha hoja kwa katibu mkuu (utumishi) ili atoe kibali cha kuongeza muda wa likizo ya uzazi. Matukio ya uzazi wa mapacha zaidi ya wawili na watoto njiti ni nadra kutokea mara kwa mara.”

“Natoa wito kwa waajiri na wasimamizi wa rasilimali watu katika utumishi wa umma kutoa taarifa kwa katibu mkuu (utumishi) kuomba kibali cha kuongezwa muda wa likizo ya uzazi kwa watumishi wa umma walio chini yao watakapojifungua watoto pacha zaidi ya wawili au watoto njiti,” amesema Mwanjelwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad