Kiingereza Kuendelea Kuwa Lugha ya Kufundishia - Waziri Ndalichako

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce amesema Kiingereza kitaendelea kuwa lugha ya kufundishia na kujifunzia katika ngazi ya elimu ya sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu.

Akijibu swali la mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM), Athuman Maige leo, Ndalichako amesema Kiingereza kitaendelea kutumika kwa sababu ya umuhimu wake kitaifa, kikanda na kimataifa kwa mawasiliano na biashara ili kuwajengea wanafunzi ufahamu na umahiri wa lugha hiyo.

“Suala la matumizi ya lugha ya kufundishia na kujifunzia ni la kisheria kama ambavyo sheria ya elimu sura 353 inavyoelekeza. Sheria hiyo inabainisha matumizi ya lugha mbili za kufundishia na kujifunzia ambazo ni Kiswahili na Kiingereza.”

“Kwa sasa Kiswahili kinatumika kufundishia katika ngazi ya elimu ya awali na msingi, vyuo vya ualimu ngazi ya cheti na vyuo vya ufundi stadi,” amesema Profesa Ndalichako.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hii inaleta Faraja Sana.
    Ukitaka kujua umuhimu Mwangalie Shish Baby anavyo I Anya na kwa shauku kubwa anavyo isema you know what awm seiying. Tuanzie toka darasa LA uchekechea.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad