Msanii wa filamu nchini Steve Nyerere amekanusha tuhuma zilizotolewa dhidi yake, kuhusiana na kutofikisha michango kwa familia ya marehemu Agness Masogange ambaye alifariki Aprili 20, 2018.
Pichani marehemu Agness Masogange akiwa na mwanaye pamoja na Steve Nyerere.
Wakizungumza na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, dada wa mzazi mwenzake Agnes, anayejulikana kwa jina la Sania, amesema kuwa mpaka sasa hawajapewa pesa yoyote, hata ile ahadi ya kumkatia mtoto bima ya afya haijafanyika.
Akizungumzia madai hayo alipotafutwa na www.eatv.tv, Steve Nyerere amesema kuwa hakuna kitu kama hicho na hawezi kufanya kitu kama hicho, aliwasilisha mchango huo wakiwa na watu wengine akiwemo mchekeshaji MC Pilipili na walimkabidhi dada wa marehemu.
"Tulikabidhi mchango ule ambao ulikuwa ni kiasi cha shilingi milioni moja na laki mbili na kinachoendelea sasa ni kikundi cha watu wachache wanaotaka kumchafua Steve Nyerere na mpaka hapa nilipofikia mimi najifananisha na Bakhresa siwezi babaika na pesa ndogondogo hizo", amesema Steve.
Steve ameongeza kuwa kinachoendelea sasa ni kupotosha umma na ukweli uliopo ni kuwa , hakukuwa na maelewano mazuri baina ya familia ya marehemu na ile ya mzazi mwenzake ambao ndio wanaodai michango kwaajili ya ada ya mtoto haijawafikia.
Mwanamitindo na video queen maarufu bongo Agnes Gerald maarufu kama Masogange, alifariki dunia Aprili 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma alipokuwa akipatiwa matibabu.
Tazama VIDEO