Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amegoma kurudi mapema Bongo endapo timu ya taifa ya Congo itapoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Zimbabwe katika michuano ya AFCON 2019 inayoendelea nchini Misri.
Zahera kwa sasa yupo na kwenye benchi la ufundi la timu ya Congo akiwa ni kocha msaidizi na timu yake ipo mkiani kwenye kundi A baada ya kupoteza michezo yote miwili kwa kufungwa na Uganda pamoja na Misri.
Zahera amesema kuwa kwa sasa hafikirii kurejea Tanzania kuanza kukikonoa kikosi chake cha Yanga badala yake atakwenda Ufarasa kula bata na familia.
“Nimkekaa muda mrefu Tanzania nikiwa na timu yangu ya Yanga, kwa sasa sifikirii kurejea mapema kuanza maandalizi kwani ni muda wangu wa kupumzika na mke wangu.
“Mchezo wangu wa mwisho utakuwa tarehe 30 nina imani ya kufanya vizuri kwani tayari kwa sasa wachezaji wamepata uzoefu na nina imani ya kushinda kama tukipoteza basi nitakwenda zangu Ufarasa kupumzika na familia,” amesema Zahera.