Kocha wa Taifa Stars Bado Anamatumaini ya Kuifunga Algeria Kesho



Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Emmanuel Amuneke anaamini timu yake ina nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo wa mwisho wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 dhidi ya Algeria hapo kesho.

Akizungumza na Waandishi wa habari mjini Cairo, Misri amesema kuwa licha ya Algeria kuwa na kikosi kizuri, lakini bado ana matumaini makubwa na vijana wake kuwa watafanya vizuri katika mchezo huo wa mwisho wa kundi C.

“Tumecheza na Algeria mara kadhaa, nakumbuka mchezo wa Dar es Salaam tuliocheza tukafungwa 2-0 na baadaye tukaja kucheza nao tukatoka nao 2-2, nakumbuka pia walikuja wakatufunga bao 7-0, lakini hiyo yote ni historia,”alisema na kuongeza:

Ameendelea kwa kusema, “Kwa sasa hivi tunachokitazama ni namna gani tutaweza kusawazisha makosa yetu yaliyotokea katika michezo miwili iliyopita na kufanya maamuzi sahihi tunapokuwa na mpira".

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad