Kumenoga, Huku Diamond Na Tanasha,Kule Mama Na Baba Yake Wa Kambo!


Video inayomuonyesha star wa bongo fleva Diamond Platnumz akicheza na mpenzi wake Tanasha Dona pamoja na mama yake staa huyo akicheza na kibenten, Rally Jones imesambaa mtandaoni na kuleta maneno.

Na hii yote ni kuelekea siku ya tarehe 7 mwezi wa saba.



Mapema wiki hii wakati akitangaza rasmi kuanza kwa Wasafi Festival ,Diamond alidai kuwa tarehe 7 mwezi huu atafanya jambo kubwa la kihistoria.



Katika video hiyo, Diamond na baba yake huyo wa kambo walikua wamevaa suti za rangi nyeusi na shati nyeupe na huku Tanasha na Mama yake Diamond wakiwa wamevaa nguo zenye rangi ya maroon, mavazi yanayofanania na ya harusi

Katika video clip aliyopost msanii Diamond Platnumz katika akaunti yake ya instagram imeonyesha kiutaratibu kabisa akicheza mtindo flani hivi wa salsa na mama yake pia akicheza mtindo huo na mumewe ajulikanaye kama Rally Jones.



Pia kulisikika sauti ambayo inakisiwa kuwa ni ya Rayvany ikiwasifia couples hao

“#707 Mlimani City July 7th 2019🔥🌍🔥,” Diamond aliandika.



Mama yake Diamond Platnumz ama Mama Dangote kama anavyojulikana amepost kipande kingine cha video katika instastory yake na kuipa caption za lyrics za tetema.

Hili limezua maneno mkanganyiko mtandaoni huku kila mtu akija na mawazo yake, cheki mwenyewe hapa chini;

princewizy
Hiii familia banaaa 😀😀 mtoto yuko guest chumba namba 8, Mama yuko namba 9
hkunasa
Kitu nisicho kipenda kwako nihuyo bwege kumdanga mama yako. Hapo alipaswa asimame mzee mwenyewe og

me.rcy4968
Umekurupuka baada ya kuona zari kaja east Africa😂😂😂kazi unayo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad