Kwa mujibu wa kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nakusema kuwa,watuhumiwa hao walikamatwa juzi baada ya jeshi la polisi kuwawekea mtego na kufanikiwa kuwakamata.
Amefafanua kuwa , siku ya tukio watu hao walifika kwenye ghala ya mfanyabiashara huyo na kujitambulisha kwake kuwa ni maafisa usalama wa Taifa na kumwomba rushwa kiasi cha shilingi Milioni tatu ili waweze kumsaidia kufungua ghala lake ambalo lilifungwa na TFDA.
Kamanda ABWAO amesema MORO alitoa taarifa kwa jeshi la polisi juu ya watu hao walifika kwake na kujitambulisha kuwa wao ni maafisa usalama wa Taifa na wanauwezo wa kumfungulia ghala ambao lililokuwa limefungwa na TFDA na kumuomba fedha hizo kama Rushwa ili kufanikisha zoezi hilo.
Maafisa Usalama Feki Wanaswa Kahama Wakitapeli Mfanyabiashara
0
June 05, 2019
Tags