Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema madakatari wote waliosoma kwa fedha za serikali watapangwa katika vituo vya kazi na serikali sehemu yeyote kwa kuzingatia mahitaji ya afya.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Faustine Ndugulile wakati akijibu la Mbunge Abdalah Chikota (CCM) ambaye alihoji juu ya kupelekwa kwa Madaktari Bingwa kwenye Hospitali za Mkoa.
“Lengo ni kuwa kila Hospitali hizi zinakuwa na madaktari bingwa wa fani nane, fani hizo ni pamoja na Daktari bingwa magonjwa ya uzazi na wanawake , Watoto, magonjwa ya ndani, upasuaji, upasuaji wa mifupa, Daktari wa huduma za dharura na magonjwa ya ajali “ amesema Ndugulile
Aidha Naibu Waziri Ndugulile amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2017/2018 Wizara iliwapeleka madaktari bingwa wa fani za upasuaji wa kawaida na upasuaji wa mifupa 125 katika Chuo cha MUHAS na wanatarajia kumaliza masomo yao katika mwaka wa fedha wa 2020/2021.