Jeshi la Polisi mkoani Arusha limekamata madini aina mbalimbali ambayo yalikuwa yakitoroshwa kuelekea nchi jirani ya Kenya.
Madini hayo zaidi ya kilo 36 yamekamatwa jana Jumatano Juni 26, 2019 na askari maalum ya intelijensia baada ya kupata taarifa madini hayo kutoroshwa kutoka Arusha katika basi la Perfect trans ambalo hufanya safari kutoka Arusha hadi Nairobi nchini Kenya.
Mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe amesema madini hayo ikiwepo Tanzanite kilo tano, Ruby na Greentonaline yalikuwa yanasafirishwa kwenye mfuko mkubwa yakiwa yamechanganywa na mchele.
Amesema dereva wa gari hilo na kondakta wake wanashikiliwa kwa mahojiano wakidai hawamjui mmiliki wa madini hayo.
Madini ya Mamilioni ya Pesa Yakamatwa Yakitoroshwa Kuelekea Kenya
0
June 27, 2019
Tags