Mahakama Yaamuru Mwanaharakati Aliyedaiwa Kumtusi Museveni Ana Kesi ya Kujibu

Mtafiti wa Chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda Dkt. Stella Nyanzi ameagizwa kujitetea katika kesi ambapo anatuhumiwa kumtukana rais Yoweri Museveni.

Ikitoa uamuzi wake mahakama iliopo katika barabara ya Baganda ilisema kuwa alikuwa na kesi ya kujibu.

Kwa mujibu wa gazeti la The Monitor nchini Uganda, baada ya kusikiza ushahidi kutoka kwa mashahidi watatu wa serikali, hakimu bi Gladys Kamasanyu aliamuru siku ya ijumaa kwamba Dkt Nyanzi, ambaye anazuiliwa katika gereza la Luzira ana kesi ya kujibu.


Baada ya uamuzi huo Dkt Nyanzi alisema kuwa atawasilisha kati ya mashahidi watano hadi saba kumtetea.

Hakimu huyo amesema kuwa mshukiwa huyo anamiliki akaunti ya ukurusa wa facebook ambao ulichapisha 'matusi' hayo.

Dkt Nyanzi anashtakiwa kwa kutekeleza unyanyasaji wa mtandaoni pamoja na kutoa matamshi machafu swala ambalo linakiuka sheria nchini Uganda.

Mnamo tarehe 9 mwezi Novemba , Dkt Nyanzi alikataa kuomba dhamana.

Hatahivyo bwana Isaac Ssemakade, wakati huo alisema kwamba mteja wake alitaka serikali kuharakisha uchunguzi ili kumwezesha kuendelea na kesi.

Upande wa mashtaka unasema kuwa mnamo mwezi Septemba tarehe 16 2018, Dkt Stella Nyanzi alichapisha katika ukurasa wake wa facebook madai yaliodaiwa kuwa machafu kwa rais Museveni na marehemu mamake.

Imedaiwa kwamba pia alichapisha ujumbe wa kuvuruga amani, utulivu na kuingilia faragha ya rais Museveni.

Hii ni mara ya pili maafisa wa polisi wanamtuhumu Dkt Nyanzi kwa madai ya kumtusi Museveni na familia yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad