Mahusiano ya kibiashara kati ya Marekani na China kuanza upya


Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa China Xi Jinping wamekubaliana kuendelea na mazungumzo ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

Kulingana na shirika la habari la Shinhua nchini China,mkutano wa G20 uliofanyika  Osaka nchini  Japan ulmesababisha kuzungumza kwa Donald Trump na Jinping.

Kwa mujibu wahabari,viongozi hao wawili walifanya mazungumzo kwa zaidi ya lisaa limoja.

Rais wa Marekani na China wamekubaliana kuwa mataifa hayo mawili yataanza upya mahusiano ya  kibiashara  na kiuchumi katika misingi yenye usawa na heshima.

Trump alisisitiza kuwa Marekani haitaweka ushuru wa ziada kwa China.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad