Mameneja TANESCO wapewa siku saba

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, ametoa Siku Saba kwa Mameneja wa TANESCO kote nchini kutembelea viwanda kwenye maeneo yao kwa lengo la kuhakikisha kuwa viwanda hivyo vinapata umeme wa uhakika kwa ajili ya uzalishaji na kufanya utatuzi endapo kutakuwa na changamoto ya kutokuwepo kwa umeme kwenye maeneo hayo.



Aliyasema hayo wakati wa Mkutano wake na Jumuiya ya Wamiliki wa Viwanda ambapo kikao  hicho kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt Hamisi Mwinyimvua, Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Salum Shamte, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye, Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, Kaimu Kamishna wa Petroli na Gesi, Mwanamani Kidaya, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt Tito Mwinuka na watendaji wengine kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara na Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI).

“Nimetoa Siku Saba za kutekeleza suala hili na kama hawajatembelea maeneo yenu, wenye Viwanda toeni  taarifa ili tuweze kuchukua hatua lakini na ninyi wamiliki wa viwanda, hakikisheni kuwa mnalipa bili za umeme la sivyo tutakata umeme.” alisema Dkt Kalemani.

Kuhusu gharama za umeme aliagiza kuwa, TANESCO waendelee kutoa  gharama halisi za kumuunganishia mteja umeme na si kulimbikizia gharama hizo hali itakayochelewesha lengo la uanzishaji wa viwanda vingi nchini.

“Mkifanya makadirio ya gharama za umeme anazopaswa kulipia mteja hakikisheni kuwa mnaweka gharama halisi kwa sababu ikitokea umeagizwa kurudia kufanya makadirio hayohayo na yakashuka, Meneja, utachukuliwa hatua.” alisema Dkt Kalemani.

Kuhusu ushirikishaji wa Sekta binafsi kwenye Sekta ya Nishati, Dkt Kalemani alisema kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana na Sekta hiyo kwani kukua kwa uchumi wa nchi kuna tegemea mashiriakiano kati ya pande hizo mbili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad