Mawigi yaleta kizaazaa Bungeni, wanaume waonywa

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Taska Mbogo amewaonya wabunge wanaume wanaoshangilia ongezeko la kodi katika bidhaa za urembo ikiwemo nywele bandia (mawigi).

Mbogo ametoa kauli hiyo wakati akichangia mjadala wa bajeti iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha Dkt. Philip Mpango ambapo Bunge limeridhia na kupitisha bajeti kuu ya nne ya serikali ya awamu tano kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Mbogo akichangia upande wa kodi zilizoongezwa ikiwemo katika bidhaa za nywele bandia 'mawigi' na rasta amesema kuwa amechukizwa na baadhi ya wabunge wanaume wanaoshangilia hatua hiyo huku wakidai kuwa watapendeza zaidi wakibaki na nywele zao za asili.

"Kuna watu wanasimama hapa kuchangia na kusema kuwa wanapenda wanawake wenye vipilipili, kila mmoja ana kitu anachokipenda kwani ni masuala binafsi zungumzeni yanayowahusu kuhusu ya wanawake tuachieni wanawake wenyewe", amesema Mbogo.

Ameongeza kuwa, "Haijalishi yatauzwa bei gani hatuwezi shindwa kununua wala kusuka tutavaa tu, hatushindwi sisi tunapambana wenyewe kutafuta pesa zetu".

Bajeti hiyo ina jumla ya shilingi trilioni 33.1. Baada ya kujadiliwa kwa siku 7 ilipitishwa na wabunge kwa kishindo huku ikiwa na ongezeko la baadhi ya bidhaa zikiwemo taulo za kike na mawigi huku kodi zingine zikipunguzwa.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad