Mbunge ahoji ushuru wa nywele bandia kupandishwa 'Kwanini wasichague bidhaa ya Wanaume?'

Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Suzan Lyimo  amewataka Wabunge wanawake kuandamana baada ya bajeti Kuu ya serikali  kuongeza  ushuru wa nywele bandia (mawigi) wa asilimia 10 kwa bidhaa za nywele bandia zinazozalishwa nchini na asilimia 25 kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje nchi.



Lyimo amesema kuwa anaona bajeti hiyo haina gender balance kwanini haijatafuta bidhaa ya wanaume waiwekee kodi? wanachagua bidhaa za wanawake?

"Mawigi ni bidhaa kwaajili ya wanawake. Kuna watu "naturally" hawana nywele, wana vipilipili hivyo ni lazima wavae mawigi, nilitegemea wabunge wanawake tuandamane kupinga hii bajeti, imekuwa "gender insensitive" hasa suala la pedi kurudishiwa kodi,"alisema Lyimo.

Hata hivyo, Mbunge huyo alitoa mfano wa baadhi ya Wabunge waliovaa mawigi walivyopendeza huku akimtaka Naibu Spika kuwaangalia

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad