MBWANA Samatta na Amunike WATOA Ujumbe Kuhusu AFCON 2019


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Emmanuel Amunike pamoja na Nahodha wa kikosi hicho Mbwana Samatta, wamesema wamefanya maandalizi mazuri kuelekea mchezo wao wa kwanza kwenye AFCON 2019, dhidi ya Senegal.



Wakiongea leo Juni 22, 2019 kambini Misri, Amunike amesema wajiamini katika maeneo yote, stamina, ufundi na kimchezo zaidi.

''Kitu cha msingi kwenye mchezo wa kesho ni maandalizi katika maeneo yote tuliyofanya na wachezaji watakuwa na hali nzuri ya kucheza katika mashindano makubwa kama AFCON na tunaamini tutafanya vizuri'', amesema.

Kwa upande wake Mbwana Samatta, amesema wanaiheshimu Senegal lakini wao pia ni timu iliyokwenda kushindana kwahiyo wataingia uwanjani kutafuta matokeo ya ushindi.

''Kucheza na mataifa kama Senegal sio rahisi, lakini ili uwe bora unahitaji changamoto kama hizi na katika mchezo kabla ya dakika 90 kila timu inakuwa na nafasi ya kufanya lolote'', ameeleza.

Tanzania kesho itatupa karata yake ya kwanza kwenye AFCON 2019 ambazo ni fainali za pili kushiriki kama taifa kwa kucheza na Senegal ambao wanashiriki kwa mara ya 15.

Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa 30 June jijini Cairo, kuanzia majira ya saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Uwanja huo una uwezo wa kuingiza mashabiki 30,000.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad