Misri yatema mchezaji kambini kwa utovu wa nidhamu

Kocha wa timu ya taifa ya Misri, Hani Abu Reda ametangaza kumtema kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Amr Medhat Warda.

Warda mwenye umri wa miaka 25, ametemwa ikiwa ni masaa machache kabla ya mchezo wa pili wa hatua ya makundi katika michuano ya AFCON inayoendelea nchini humo, mchezo ambao utapigwa leo dhidi ya Congo DR majira ya saa 5:00 usiku.

Imetajwa kuwa nidhamu mbovu ndiyo sababu za kuachwa kwake, ambapo kwa mujibu wa mitandao mbalimbali nchini Misri, mchezaji huyo amehusika katika unyanyasaji dhidi ya mwanamitindo raia wa nchi hiyo, Merhan Keller.

"Hani Abu Reda amefikia uamuzi huo baada ya kuwasiliana na benchi la ufundi ili kulinda nidhamu katika kambi ya timu. Timu ya taifa itamaliza ratiba iliyobaki ya mashindano na idadi ya wachezaji 22", imesema taarifa kutoka katika tovuti ya chama cha soka nchini humo.

Warda ni kiungo mshambuliaji katika klabu ya PAOK ya nchini Ugiriki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad