Mizinga ya Bar Maids Sehemu za Starehe Inauzi



Niende moja kwa moja kwenye mada,
Kuna tabia ya bar maids karibia wote kuomba uwanunulie kinywaji hasa pale anapoona umekunywa pengine bia tatu na kuendelea.

Mara nyingi unapoagiza labda bia ya tatu au ya nne unakuta anakwambia "kaka/uncle vipi Mimi sinywi hata moja?" Au "kaka Mimi hata soda tu" au "Chenji si na Mimi ninywe soda?"

Hii adha nimekuwa nikikutana nayo Mara nyingi sana. Mwanzoni nilikuwa naona fresh tu baadae nimeona kumbe ni tabia yao karibia wote.
Kwa kifupi imekuwa kama ni haki yao kupewa kinywaji au uwaachie chenji na usipowapa basi siku nyingine ukienda hawakuchangamkii kukuletea huduma, sasa unajiuliza yeye yupo pale kwa kazi gani kama anachukia mteja asiyempa ofa au anayedai chenji?
Mfano Jana nilikuwa sehemu Fulani nimeagiza kinywaji nikakuta wahudumu wanamjadili mteja mmoja aliyefika. Mmoja ya wahudumu hao nilimsikia akisema " Akhaaa nenda kamhudumie wewe mi nasubiri wengine, mteja bahiri kama nini"!. Walinikera na nikawaeleza waziwazi kwamba kwa kufanya hivyo hawajui wajibu wao.

Kuna muda huwa nawapa tu na muda mwingine unakuta nina kahela ka bia mbili au tatu tu nimeamua nikapoze koo kidogo ila wao huwa hawatambui hilo. Naamini adha hii inakuta wenzangu wengi tu ila huwa hawasemi

NB: nimesema hili siyo kwa sababu mi mchoyo Bali hawa wauzaji kwenye Bar,Groceries au Pubs wanapaswa kutambua kuwa si haki yao kununuliwa vinywaji au kuachiwa chenji na Mara nyingine mteja anaenda kuwaunga mkono huku akiwa hayuko vizuri. Ili kukomesha hili wanywaji wenzangu muwe mnawaelimisha Hawa wahudumu hasa pale unapokutana na adha za namna hii.
Mwisho kuwasilisha,samahani kwa wale nilowakera kwa hili.


Severinembena
JF
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad