Mke wa Makamu was Rais Ataka Mahari za Wanawake Zishushwe

Wazazi Nchini wametakiwa kutowafanya watoto wao wa kike kuwa chanzo cha mapato, kwa kuwawekea kiwango kikubwa cha mahari pindi watakapokuwa wakihitaji kuolewa akidai kuwa suala hilo husababisha vikwazo kwa vijana wa kiume wanaotaka kuoa.


Kauli hiyo imetolewa na mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Asha Suleiman Iddi akiwa visiwani Zanzibar katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya Qaswida.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mama Asha amesema, "nawahasa wazazi wenzangu, msiwatumie vijana wenu wa kike kama chanzo cha mapato, mnawawekea mahari kubwa sana, mnasababisha vijana wakiume washindwe na waogope kujitokeza kuwaona".

Awali akisoma risala muandaaji wa mashidan hayo, Mwashaban Seif Ali amesema mashindano hayo yameanza kuonyesha muelekeo wa kukubalika ndani ya jamii kutokana na ongezeko kubwa la washiriki kutoka Madrasa 10 Mwaka 2018 na kufikia hadi Madrasa 20 kwa Mwaka 2019.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad