Mkuu wa Wilaya apambana na wachawi njia panda

Kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ushirikina katika eneo la Njiapanda inayoelekea nyumbani kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamringi Macha, imeelezwa kuwa watahakikisha unawekwa ulinzi maalumu  ili kuweza kuwabaini na ikiwezekana kuwakamata watu  wote wanaofanya ushirikina huo.


Mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamringi Macha

Macha amesema kukithiri kwa vitendo hivyo, kumepelekea uharibifu wa mazingira na kwamba eneo hilo limekuwa likifanyiwa shughuli za kishirikina kwa kuchinja kuku na kutupa vitu vyenye mchanganyiko mbalimbali pasipo kujua vina athari kiasi gani kiafya.

''Ni kwa Muda mrefu vitendo hivyo vimekuwa vikifanywa hapo na nilipotoa taarifa hii watu wakahisi labda kwa vile ni njia inayoelekea kwa Mkuu wa Wilaya, hapana ni kwa vile ni eneo lao ambalo wanaliona kama linafaa kwa shughuli hizo na hivyo uharibifu wa mazingira unatokana na ule uchafu tunaoukuta mara kwa mara''.

Mkuu huyo wa wilaya, amesema ijapokuwa ni jambo kama la kufurahisha hivi na watu wengi wanaamini kuwa haitowezekana kwa jamii kuamini kwamba hata wakiweka doria hawatoweza kuwakamata hii ni kutokana na imani walizojiwekea.

Hivyo amesema kutokana na hali hiyo asingependa kuona mazingira yanachafuliwa kwa kiasi hicho, kulingana na imani potofu zisizokuwa na tija  ambayo jamii imejiwekea na kwamba wananchi waelimishwe ili kuweza kuondokana na dhana hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad