WIKI imekuwa ya neema kwa msanii wa Bongo Fleva ambaye pia ni muuza nyago katika video hizo, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ baada ya kutinga mjengoni, Global Group, Sinza-Mori jijini Dar na kuwataja mastaa waliomshangaa uwezo wake alipoachia wimbo wake wa kwanza wa Watakoma.
Akifanyiwa Exclusive Interview na radio janja namba moja kwa sasa Bongo ya +255 Global Radio kupitia kipindi cha Bongo 255, Amber Lulu aliyewahi kutikisa na vibao vingi ikiwemo Watakoma alisema kwamba, siku ya kwanza kujitambua anaimba aliingia studio na kuibuka na wimbo wa Watakoma.
“Mimi kufanya muziki imetokea tu katika kutafuta riziki, sikuwa najua kama nina kipaji zaidi ya kuimbaimba tu. Ndoto yangu kubwa ilikuwa kuwa mbunifu mkubwa lakini sikufikiria kuimba. Siku ya kwanza kuingia studio ndiyo siku hiyohiyo nikaachia Wimbo wa Watakoma na ukapaa,” alisema Amber Lulu na kuongeza.
… Akiwa katika pozi ndani ya Studio za +255 Global Radio.
“Kwanza idea ya kufanya Watakoma ilitoka kwa Mose Thomas (Swesweka) na mtu wa kwanza kumtambulisha alikuwa Country Boy hakuamini, tukaingia studio akaingiza sehemu yake siku hiyohiyo. Baada ya hapo sasa sikuamini kilichoendelea kunitokea kwani mastaa kibao waliposikia wimbo wangu wa Watakoma kila mmoja alitamani kufanya na mimi kazi akiwemo Billnass. Mr Blue simu zilikuwa nyingi hadi watu wengine nilikuwa siamini kama wanaweza kunipigia,” alisema Amber Lulu.
Alielezea pia staa wa muziki kutoka Kenya, Prezzo, anavyokwamisha kumalizia video ya wimbo wake mpya wa Makeke.
“Video nimeshaanza kuchukua vipande Nairobi na Bongo lakini kinachofanya hadi sasa video yangu ikwame ni Prezzo, yupo mbali kwa hiyo tunachukua vipande tunatulia tunachukua tena kama mjuavyo kwenye video kuna mambo mengi. Kuna vipande nimepiga na Prezzo huko Nairobi japo havijapendeza sana,” alimaliza kusema Amber Lulu.
Kwa mahojiano zaidi unaweza kutembelea Mtandao wa Youtube na kutafuta Global TV Online. Pia unaweza kusikiliza Global Radio kwa kupakua APP ya 255 Global Radio katika Playstore kwenye simu yako.
Imeandikwa na: Andrew Carlos/GPL