Kuna ushahidid kamili kwamba mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman na maafisa wengine wa ngazi za juu wanahusika kibinafsi kwa muaji ya Jamal Khashoggi, kulingana na mtaalamu wa Umoja wa mataifa.
Ripoti ya mtaalamu huyo wa UN Agnes Callamard inasema kuwa ushahidi huo unahitaji kufanyiwa uchunguzi na jopo huru la kimataifa lisilipoendelea upande wowote.
Khashoggi aliuawa katika ubaloizi wa Saudia mjini Instanbul na maajenti wa Saudia.
Watawala wa Saudia wanasisitiza kuwa wauaji wake hawakutumwa na mwanamfalme Mohammed.
Ufalme huo wa Ghuba umeweka washukiwa 11 wasiojulikana katika jopo kujibu mashtaka na tayari imewawekea hukumu ya kifo watano kati yao.
Hatahivyo bi Callamard alisema kuwa jopo hilo lilishindwa kuafikia viwango vya kimataifa na kulitaka kuvunjiliwa mbali.
Je Jamal Khashoggi aliuawa vipi?
Mwandishi huyo aliyekuwa na umri wa miaka 58 , na aliyekuwa akiandikia gazeti la the Washington Post na mkosoaji mkubwa wa mwanamfalme Mohammed mara ya mwisho alionekana akiingia katika ubalozi wa Saudia tarehe 2 Oktoba ili kuchukua nakala alizohitaji ili kumuoa mchumba wake Hatice Cengiz.
Bi Callamard , mtaalamu huyo wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya kiholela alisema kuwa Khashoggi aliuawa kikatili ndani ya ubalozi huo.
Shalaan Shalaan aliambia maripota kwamba mnamo mwezi Novemba kwamba mauaji hayo yaliagizwa na kiongozi wa wapatanishi aliyetumwa mjini Instanbul na naibu afisa mkuu wa ujaususi ili kumlazimisha Khashoggi kurudi katika ufalme huo kutoka mafichoni kwake.
Wachunguzi waliamua kwamba Khashoggi alilshikwa kwa nguvu baada ya kukataa na kudungwa sindano iliokuwa na kiwango cha juu cha dawa hatua iliosababisha kifo chake'', alisema bi Shaalan .
''Mwili wake baadaye ulikatwakatwa na kupatiwa mshirika wa ajenti hao nje ya ubalozi'' , aliongezea.
Watu watano tayari wamekiri kumuua, bi Shaalan alisema akiongezea '' mwanamfalme hakuwa na habari kuhusu hatua hiyo''.
Ripoti hiyo inasema nini?
Mnamo mwezi Januari afisi ya haki za kibinaadamu katika Umoja wa Mataifa ulimpatia bi Callamard jukumu la kuchunguza kuhusu kiwango cha utaifa na watu binafsi waliohusika katika mauaji hayo.
Maafisa waandamizi wa Saudia wanasisitiza kuwa kifo cha Khashoggi kilitokana na operesheni mbaya , lakini mchunguzi huyo wa UN anasisitiza kuwa ni mauaji ya kiholela ambapo ufalme wa Saudia unadaiwa kuhusika
Mwana Mfalme wa Saudia Kuchunguzwa Kisa Mauaji ya Mwandishi Jamal Khashoggi
0
June 19, 2019
Tags