Mwanamke mjamzito ashitakiwa kifo cha mwanawe aliyeuawa kwa kupigwa risasi akiwa tumboni

Mwanamke wa miaka 27 kutoka jimbo la Alabama, nchini Marekani ameshitakiwa kwa kuua bila kukusudia baada ya kupoteza ujauzito katika kisa cha ufyetulianaji risasi.

Marshae Jones alikamatwa siku ya Jumatano kwa kuhusika katika mzozo uliosababisha apigwe risasi ya tumbo, vyombo vya habari vinaripoti.

Mashataka dhidi ya Ebony Jemison aliyempiga risasi yalifutwa na mahakama kwa mdai kuwa alifanya hivyo kujilinda.


Makundi ya kutetea haki yanasema kuwa hatua hiyo inaonesha kuwa sheria mpya za jimbo hilo zinazodhibiti uavyaji mimba zitaathiri kesi zingine.

Bi Jones alipigana na Ebony Jemison mwenye umri wa miaka 23, tarehe 4mwezi Desemba mwaka jana, akiwa na ujauzito wa miezi mitano, kwa mujibu wa AL.com

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad