Nyota wa Brazil Neymar alienda katika kituo cha polisi mjini Rio de Janeiro kuwasilisha taarifa kufuatia madai ya ubakaji , kulingana na wakili wake.
Nyota huyo amekana kumbaka Najila Trindade katika hoteli moja mjini Paris mnamo tarehe 15 mwezi Mei na kuwashukuru mashabiki wake nje ya kituo kwa usaidizi wao.
Bi Trindade aliwasilisha madai hayo Ijumaa iliopita akiambia runinga moja ya Brazil kwamba alikuwa anataka haki kutendeka.
Kampuni hiyo ya kuchukua fedha kwa mkopo imesema kuwa itasitisha utumizi wa picha za nyota huyo, ambaye ndio mchezaji aliyesajiliwa kwa kitita kikubwa cha fedha na anaichezea klabu ya PSG hadi pale tatizo hilo litakapotatuliwa.
Kampuni ya jezi za michezo Nike nayo ilikuwa imetangaza kwamba ina wasiwasi kuhusu madai ya ubakaji dhidi ya Neymar, ambaye inamfadhili.
Anasema kwamba wakati walipokutana na Neymar alikuwa mtu wa fujo ''mtu tofauti na yule niliyemjua katika ujumbe''.
Bi Trindade alikua amejiandaa kushiriki ngono lakini akataka watumie mipira ya kondomu. Anadai kwamba Neymar alikataa akaleta fujo na kumbaka.
Anasema kwamba alimwambia kuacha kufanya hivyo lakini akakataa.
SBT ilichapisha baadhi ya mahojiano hayo katika mtandao wa Twitter { kwa Kireno).
Ni nini kilichotokea katika kituo cha Polisi?
Neymar aliwasili katika kituo cha polisi kwa kutumia magongo baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu wakati wa mechi ya Brazil dhidi ya Qatar mjini Brasilia siku ya Jumatano.
Wakili wake , Maira Fernandes aliambia Rueters : Neymar ametoa taarifa .
''Alichukua hatua ya kuja haraka ili kutoa taarifa , ili kuweka uwazi kila kitu kilichohitajika kuwekwa wazi''.
''Tuna matumaini kwamba tutahakikisha kua mteja wetu hana hatia. Mkakati ulikuwa mrefu lakini alitoa ufafanuzi uliohitajika''.
Akizungumza katika mlango wa kituo cha polisi, Neymar alisema: Nathamini usaidizi niliopata na ujumbe wote ambao ulimwengu umenitumia, marafiki zangu, mashabiki wangu, na ulimwengu uko nami. Nataka kusema ahsante sana kwa ujumbe huo wa kunipa moyo na nahisi kwamba ninapendwa sana''.
Neymar Awasilisha Taarifa kwa Polisi Kufuatia Madai ya Ubakaji
0
June 07, 2019
Tags