Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Nikki wa Pili amesema kuwa mfumo wa sasa wa mwanaume kuonekana ndio kichwa cha familia ni mbaya na hautakiwi kuendelezwa kwani unafanya mwanaume kuchoka haraka.
Nikki wa Pili na mkewe.
Nikki wa Pili amedai kuwa kwenye familia lazima kuwe na usawa wa kijinsia ili wanawake na wanaume wote wawe na haki sawa ya kuijenga familia.
Akitolea mfano wa familia yao, Nikki amesema kuwa Baba yake mzazi alikuwa ndio kichwa cha familia jambo ambalo lilifanya yeye kuwa mtu wa mwisho kutoa maamuzi.
“Baba yangu alikua kichwa cha familia mwamuzi wa mwisho, mm nataka kua baba wa familia ambayo wazazi wote wawili ndio vichwa vya familia na wanaamua kwa kukubaliana, Mzee wangu ni picha halisi ya mfumo dume mimi nataka kua picha halisi ya usawa wa jinsia.” ameandika Nikki wa Pili kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Nikki amesema kuwa mfumo dume ndio chanzo cha akinja baba wengi kupoteza maisha haraka kutokana na mlindikano wa majukumu na msongo wa mawazo, jambo linalopelekea kuongezeka kwa wajane.
“Mfumo wa ubaba kama kichwa/mtafutaji mkuu, mjenzi wa mali za familia, mbeba mizigo yote, ni mfumo hatari zaidi kwa baba na ndio mana wajane ni wengi zaidi, mzigo wote huo lazima mbio za maisha ziwe fupi, ubaba bora utaletwa na usawa wa jinsia utakao punguza mzigo kwa baba mfalme,”ameandika Nikki wa Pili.
Nikki wa Pili achukizwa na mfumo wa baba kuwa kichwa cha familia '‘Tubadilike, Ndio Maana wmWajane Wanaongezeka"
0
June 18, 2019
Tags