Halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe imeendelea kutekeleza kwa vitendo agizo la serikali la kusimamia zoezi la ukusanyaji wa mifuko ya plastiki katika kata zake zote ikiwa ni kuunga mkono katazo la matumizi ya mifuko hiyo ili kuhifadhi mazingira.
Mapokezi ya wananchi juu ya katazo hilo yamekuwa makubwa, ambapo watu mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara na watu wengine wamejitokeza kwnenye kampeni maalumu ya wilaya, wakiimba nyimbo mbalimbali huku wakisalimisha mifuko yao.
Zoezi hilo limesimamiwa na viongozi wa halmashauri akiwemo Afisa Mazingira wa Wilaya ili kuhakikisha mifuko ya plastiki, maarufu kama 'rambo' ikikusanywa pamoja na wananchi kupewa tahadhari juu ya adhabu kali kwa yeyote atakayebainika kuwa na mifuko hiyo.
Ally Kassinge ni Mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe ambae anasimamia zoezi la ukusanyaji wa mifuko ya rambo katika kata zote za wilaya hiyo huku akitoa angalizo kwa raia atakae bainika na mifuko ya rambo katika maeneo yoyote ndani ya wilaya yake.
Zoezi hili la usalimishaji wa mifuko ya Rambo lina ambatana na zoezi la zoezi la kufanya usafi wa mazingira na leo katika maeneo mbali mbali wilayani humo, ambapo usafi huo umechukua nafasi katika maeneo yanayoizunguka hospitali hiyo teule ya Ilembula.