Onyo jipya kwa wanaotumia mifuko ya mikate

Baraza la Uhifadhi wa Mazingira nchini NEMC limesema halitamvumilia mtu ambaye atabainika kutumia mifuko ya plastiki ambayo imepigwa marufuku na Serikali na kueleza kuwa atakayebainika atahukumiwa kwa mujibu wa sheria inavyosema.


Kauli hiyo imetolewa na Wakili wa NEMC, Vincent Haule wakati akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast, cha East Africa Radio ambapo aliulizwa swali kuhusiana na vifungashio vya mikate kutumika kama vifungashio vya bidhaa nyingine.

Mtangazaji Charles William - "kwa watumiaji wa mikate, vipi baada ya kutumia mkate akaamua kutumia mfuko wake kufungia kitu kingine?"

Akijibu swali Wakili wa NEMC, Vincent Haule amesema, "mtu atakayejaribu kufanya hivyo anahitaji adhabu kubwa kwa mujibu wa sheria, atakuwa amefanya kosa kwa makusudi, atatozwa faini ya laki 2."

Mtangazaji Charles William  - kuhusu vifungashio mnachanganya watu, leo mnasema vioneshe bidhaa iliyopo na vithibitishwe na TBS?

Vincent Haule -  Kama mwanzo sikusema ni kosa letu, vifungashio vitaje bidhaa iliyopo, kwa mjasiriamali wa ubuyu haitamuathiri sababu si mtengenezaji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad