Ozil Afunga ndoa, Rais wa Uturuki Awa Mpambe Wake

Rais Recep Tayyip Erdogan alimsaidia mchezaji wa Arsenal Mesut Ozil kufunga ndoa na mpenziwe mjini Instabul Uturuki

Ozil, ambaye chimbuko lake ni Uturuki, ali zuahisia kali alipopiga picha na rais wa Uturuki Erdogan kabla ya kombe la dunia mwaka uliopita.

Baadaye alistaafu katika soka ya kimataifa , akidai ubaguzi wa rangi na kutoheshimiwa baada ya picha hizo kusambaa nchini Ujerumani.


Wanandoa hao walianza kuchumbiana 2017 na kutangaza kilichokuwa kikiendelea kati yao mwezi Juni 2018.

Ozil alitangaza mwezi Machi mwaka huu kwamba alimuomba rais Erdogan kuwa mshenga wake swala ambalo lilizua hisia kali nchini Ujerumani.

Helge Braun, waziri wa Chansela wa Ujerumani Angela Merkel aliambia gazeti la Bild kwamba ilikuwa uchungu sana kumuona Ozil akimchagua kiongozi kama huyo baada ya shutuma alizopata na rais huyo wa Uturuki mwaka uliopita.


Hatua yake ya kuhudhuria harusi ya Ozil inajiri wakati ambapo uchaguzi wa marudio wa Meya unasubiriwa mjini Instanbul.

Matokeo ya awali yalionyesha kwamba mgombea wake wa chama cha APK alishindwa kwa kura chache hatua iliopelekea uchaguzi huo kufutiliwa mbali na hivyobasi kuzua hisia kali za kimataifa.

Ni nini kilichotokea mwaka uliopita?
Raia huyo wa kizazi cha tatu cha Ujerumani na Uturuki alizaliwa katika mji wa Gelsenkirchen na alikuwa kiungo muhimu wa timu yataifa ya kombe la dunia ilioshinda 2014

Ameichezea Ujerumani mara 92 na mashabiki wamempigia kura kuwa mchezaji bora wa timu ya taifa mara tano tangu 2011.

Lakini mnamo mwezi Mei Ozil alizua hisia kali nchini Ujerumani alipopiga picha na rais wa Uturuki kabla ya kombe la dunia la 2018 nchini Urusi na kuwafanya wengine kujiuliza maswali kuhusu taifa analolitii.

Lakini ukosoaji huo ulizidi baada ya timu ya taifa ya Ujerumani kubanduliwa katika mashindano hayo katika raundi ya kwanza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad