Polepole Asema Wabunge Wa Ccm Wanaoleta Nongwa Kwenye Ununuzi Wa Korosho Watakatwa Majina Yao Uchaguzi 2020.


Na Bakari Chijumba, Mtwara.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg.Humphrey Polepole amesema wabunge wa CCM wenye nongwa kila serikali inapotatua tatizo, ikiwemo mchakato wa kununua korosho,watakuwa na hali mbaya Uchaguzi wa 2020, huku akiwataka watafute kazi nyingine kwakuwa watakatwa majina yao.

Akizungumza mjini Mtwara, kwenye Mahafali ya Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo na vyuo vikukuu (UVCCM) mkoani Mtwara, June Mosi,2019, Polepole amesema  Korosho ni zao linaloleta pesa nyingi nchini lakini mabeberu wanalitumia kama fimbo ya kuwachapia Watanzania.

"Korosho ni zao linaloleta pesa nyingi,ila nalo haliko salama dhidi ya Mabeberu wanatumia kama fimbo ya kutuchapia,Rais Magufuli ameamua vizuri tumenunua, ila kuna Wabunge wanazingua 'ooh hela ya kununulia korosho imetoka wapi'..hawa upinzani 2020 wajipange tutawachapa watafute kazi nyingine" amesema Polepole na kuongeza kwamba;

"Na nyie Wabunge wa CCM acheni kuwa sehemu ya tatizo,Kama wewe ni mbunge wa CCM na unashiriki kuweka Nongwa kwenye suala hili la korosho jipange mapema...Mwaka 2020 kuna michakato kadhaa ya kukata majina ya watu na kwenye michakato yote ya ukatataji mie nimo"

Polepole amesema wapo baadhi ya wabunge wa CCM  ambao wanaongeza matatizo badala ya kutatua na kusema mtu ambaye ataonesha utovu wa nidhamu hana nafasi  kwenye chama cha mapinduzi.

"Kuna wabunge wa CCM hawana nidhamu na kuna baadhi yao tunawalia Timing tu,kama kumchinja kobe acha waendelee kuruka ruka kama Bisi..Haiwezekani kila mtu anainua kichwa kama kambare kujifanya ana ndevu,Kama haufuati utaratibu kwenye CCM hauna nafasi" amesema Polepole huku akitoa msisitizo  kwa wizara kupeleka pembejeo mapema kwa wakulima.

"Sasa hivi watu wanafanya parizi ya Korosho watu wa bodi ya mazao mchanganyiko na Wizara ya Kilimo,hakikisheni Sulphur isichelewe,Pembejeo ni muhimu sana kwa Korosho zetu..Zile korosho tulizonunua bado tunaendele kuzitafutia utaratibu" amesema Polepole.

Katika hatua nyingine Polepole amezungumzia kukosekana kwa uwepo wa safari za Ndege kutoka ATCL  na kusema amewasiliana na Mkurugenzi na zitaanza kutua hivi karibuni.

"Nimempigia simu Mkurugenzi wa Air Tanzania nimemuambia nipo Mtwara ndege haziji hapa, tickets unakatia ofisi za ATCL halafu unafaulishwa kwenda Precion Air..Nimemuambia kabla ya wiki hii Ndege zianze safari za Mtwara na amelipokea, hivi Punde zitatua" amesema Polepole huku akiwapiga dongo wapinzani akidai wanapinga kila kitu ikiwemo mchakato  wa manunuzi ya Ndege.

"Bombadier inabeba watu 84 ila bado upinzani wazee wa kupinga kila kitu wakaziita bajaji..Tukanunua nyingine wakasema injini yake mbovu ndio maana ilipoinga uwanjani ikapigwa maji na magari ya fire kuipoza,wakati ni  kawaida Ndege mpya kupokelewa kwa kumwagiwa Maji".
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad