Rais wa Zamani wa Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa), Michel Platini, Amekamatwa na Polisi

RAIS wa zamani wa shirikisho la soka Ulaya (Uefa),  Michel Platini,  amekamatwa ikiwa ni sehemu ya uchunguzi unaoendelea dhidi ya madai ya kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika uamuzi wa kukubali michuano ya Soka ya Kombe la Dunia ya mwaka 2022, kufanyika Qatar.



Mcheza soka huyo wa zamani, amekamatwa mapema leo na kuwekwa kizuizini huko Nanterre, Paris, nchini Ufaransa



Platini, aliyeongoza Uefa tangu mwaka 2007 hadi 2015, kwa sasa atumikia zuio la kutojihusisha na soka kwa miaka minne baada ya kukutwa na hatia ya kupokea rushwa kutoka kwa rais wa zamani wa shirikisho la soka duniani  (FIFA), Sepp Blatter



Katika hali inayodaiwa kuwa ni ya kushangaza, mnamo Desemba 2010, Qatar ilishinda na kupewa idhini ya kuandaa michuano hiyo ya mwaka 2022.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad