RC Mwanri Aagiza Afisa Mazingira Kuchukuliwa Hatua

Mkuu wa mkoa wa Tabor,a Aggery Mwanri amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo kupitia Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kaliua kumchukulia hatua za kinidhamu, Afisa usafi na mazingira wa wilaya ya Kaliua, Abdalah Ramadhaani kwa kushindwa kusimamia ujenzi wa duka la kuuzia dhahabu katika Kata ya Chilambo wilayani humo.

Amechukua hatua hiyo baada ya kushindwa kuanza ujenzi wa duka la kuuzia madini ambayo yanachimbwa katika mchimbo ya Nsungwa Kata ya Chilambo jambo linalo kwamisha juhudi za serikali.

Katika mchimbo hayo tokea serikali ilipotoa utaratibu wa kununua madini kupitia maduka maalumu ambayo hushuhudiwa na Maafisa wa serikali tayari kilo gramu 562.9 za dhahabu vimekwisha nunuliwa.

Abel Busala ni  Mkuu wa Wilaya ya Kaliua wamewataka wachimbaji wa madini wilayani humo kufuata sheria na kanuni za biashara ya madini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad