Rostam ameyasema hayo leo mchana wakati akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Katika mkutano huo na waandishi, Rostam amesema hakubaliani na suala la mtu mmoja kumiliki klabu hiyo au kufadhili, badala yake anaunga mkono udhamini.
“Mtu mmoja amiliki klabu kubwa kama Yanga, yenye wanachama mamilioni. Hili si sahihi, hata ufadhili ni nia ya mango wa nyuma kuimiliki klabu,” alisema.
“Kwangu binafsi nitaendelea kuisaidia Yanga kama shabiki na mwanachama. Kikubwa ni uongozi kuangalia namna ya kufanya mambo yaliyo sahihi lakini si umiliki kutoka kwa mtu mmoja.
“Yanga inaweza kuingiza fedha zake kupitia udhamini, matangazo ya runinga lakini pia suala la kuuza bidhaa zake kama jezi na kadhalika,” alisisitiza.