RPC Afunguka Ajali iliyounguza Magari Mawili Baada ya Kugongana


Gari mbili za mizigo, moja lenye namba za usajili scania T182 DCM lililokuwa linatokea Iringa kwenda Dar es salaam zimegongana uso kwa uso eneo la Ruvu mkoani Pwani, na kutekea kwa moto.


Kwa taarifa za awali bado haijafahamika kama ajali hiyo imesababisha kifo cha mtu yeyote.

Akizungumza na www.eatv.tv Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa  amesema wakati tukio linatokea yeye alikuwa kanisani hivyo atafutwe majira ya saa 7 mchana atakapokuwa ametoka kanisani ndipo atoe taarifa kamili.

"Wewe ndiyo unanipa taarifa kwa mara ya kwanza, kwa sababu niko kanisani itakuwa wasaidizi wangu wameshafika eneo la tukio, kwa hiyo naomba unitafute saa 7 mchana, nikiwa nimeshatoka kanisani na nitakupa taarifa kamili." amesema RPC Wankyo Nyigesa.

Www.eatv.tv inaendelea kufuatilia taarifa zaidi za ajali hiyo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad