Rungwe Matatani aitwa Polisi Oysterbay


Dares Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Umma (Chaumma), Hashim Rungwe ametakiwa kuripoti kituo cha Polisi Oyesterbay kesho Jumatatu Juni 3, 2019.

Wito huo umekuja muda mfupi baada ya Rungwe akiwa miongoni mwa wawakilishi wa vyama vya upinzani vinane kumaliza mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Chaumma Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Wawakilishi wengine walikuwa wakitoka kwenye vyama vya Vyama vya ACT Wazalendo, CCK, Chadema, DP, NCCR Mageuzi, NLD na UPDP.

Katika mkutano huo, viongozi wa vyama hivyo walitoa tamko la kutoshiriki kwenye uchaguzi wa marudio utakaofanyika katika kata 32 Juni 15, 2019, kwa madai unasimamiwa na Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya na Manispaa kinyume na uamuzi wa Mahakama Kuu.

Alipoulizwa kwa simu, Rungwe alikiri kupokea wito huo wa Polisi.

“Ni kweli nimepewa wito natakiwa kuripoti kituo cha Polisi Oysterbay kesho saa 4 asubuhi,” alisema.

Mwananchi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad