Serikali Yaandaa Mwongozo Wa Msamaha Wa Matibabu Kwa Makundi Tofauti Yasiyokuwa Na Uwezo



Serikali kupitia wizara afya ,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto imeandaa mwongozo wa msamaha kwa makundi tofauti yasiyokuwa na uwezo ikiwa ni pamoja kundi la watu wagonjwa sugu ikiwa ni pamoja na selimundu

Hayo yamesemwa  Juni 10 ,2019 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii ,jinsia,wazee na Watoto,Dokta Faustine Ndugulile,wakati  akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum Taska Mbogo aliyehoji mpango wa Serikali wa kuwasaidia wagonjwa wa Selimundu[Sickle cell] juu ya kupata matibabu bure.

Katika Majibu yake,Mhe,Ndugulile amesema wagonjwa wa Selimundu wanahitaji matibabu mfululizo kwani huwa wanapata maumivu na madhara  ya ugonjwa huo mara kwa mara hivyo ,serikali  imeandaa mwongozo wa kutoa msamaha kwa makundi tofauti yasiyo na uwezo  ikiwa ni pamoja na kundi la wagonjwa wa Selimundu na kinachotakiwa ni kuhakikiwa na kupatiwa kibali cha huduma bila malipo.

Aidha,Dokta. Ndugulile amesema Serikali imeanzisha mpango wa Taifa wa Udhibiti wa Magonjwa yasiyoambukizwa  ambapo ugonjwa wa  Selimundu [sickle Cell] utakuwa ni moja ya magonjwa yatakayokuwa yanaratibiwa kitaifa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad