Serikali imesema imeanza ukarabati wa mashimo na kupanua barabara ya Dar es salaam,Morogoro hadi Dodoma ambayo ni kiungo muhimu kwa uchumi wa tanzania.
Naibu waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe,Elias Kwandikwa amebainisha hayo Juni 20,2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Wingi Juma Kombo aliyehoji serikali ina mpango gani wa kukarabati mashimo pamoja na kuipanua barabarahiyo.
Katika Majibu Yake Naibu waziri wa ujenzi ,uchukuzi na mawasiliano Elias Kwandikwa amesema Serikali imeanza ukarabati mashimo na kupanua barabara ya Dar eS Salaam,Morogoro hadi Dodoma ambayo ni kiungo muhimu kwa uchumi Wa Tanzania ambapo mkataba wa kazi ya upanuzi wa madaraja ya Kibamba,Kiluvya na Mpiji ulishasainiwa tangu tarehe 13,Julai,2018 na mkandarasi ESTIM Construction.Co.Ltd kwa gharama ya Sh.Bil.440,Mil.449 ,laki 5 na 21elfu.
Aidha,Mhe.Kwandikwa amesema Ukarabati wa maeneo yaliyoharibika unafanyika kwa kuondoa lami ya zamani na kuweka tabaka jipya katika maeneo ya Kibaha hadi Chalinze ambapo mkoa wa Pwani imetenga Tsh.Bil.2.5.
Hata hivyo Serikali imetenga Tsh.Milioni 800 katika mwaka wa Fedha 2018/2019 ili kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajiliya ukarabati Barabara ya Morogoro -Dodoma [km 256]
Katika hatua nyingine Mhe.Kwandikwa amesema mkandarasi yeyote atakayechelewesha kazi atachukuliwa hatua na lipia gharama za usumbufu ambapo kuna mashauri 20 ya Makandasi waliofanya uzembe
Serikali Yaanza Ukarabati Mkubwa wa barabara ya Dar es salaam,Morogoro hadi Dodoma
0
June 21, 2019
Tags