Serikali imepata fedha kutoka serikali ya india kiasi cha dola za marekani milioni 500 kwa ajili ya kuboresha huduma ya miundombinu ya maji katika miji 28 ya tanzania na Zanzibar.
Hayo yamesemwa leo Juni 19,2019 bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso wakati akijibu swali la mbunge wa Kilombero,Peter Lijualikali aliyehoji,serikali ina mpango gani wa kuongeza mtandao wa Maji.
Akijibu Swali hilo,Naibu waziri wa maji Mhe.Aweso amesema Katika mpango wa Muda Mrefu,serikali imepata fedha kutoka serikali ya India kiasi cha Dola za Marekani Milioni 500 kwa ajili ya kuboresha huduma ya miundombinu ya maji katika miji 28 ya Tanzania bara na Zanzibar ambapo mji wa Ifakara ni miongoni mwa miji itakayopata maji kupitia fedha hizo na sasa taratibu za kuwapata wataalam washauri watakaofanya usanifu wa kina na maandalizi ya makabrasha unaendelea.
Hata hivyo ,Mhe Aweso amesema kukamilika kwa mipango hiyo kutaboresha hali ya upatikanaji wa Maji kwa asilimia 90%.
Serikali Yapata Dola za Marekani Milioni 500 Kutoka India Kwa Ajili ya Kutekeleza Miundombinu Ya Maji
0
June 19, 2019
Tags