Shambulizi Kwenye Kituo cha Upekuzi Laua Polisi Kumi Nchini Misri

Maafisa wa usalama nchini Misri wamesema leo wapiganaji wa makundi ya kiislam wamekishambulia kituo kimoja cha upekuzi kaskazini ya rasi ya Sinai na kuwauwa polisi 10.

Maafisa hao wamesema shambulizi hilo limetokea mapema asubuhi ya leo wakati waislam katika mji wa al-Arish walipokuwa wakiendelea na ibada ya sikuu ya Eid al-Fitr inayosherehekewa baada ya kumalizaka kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Hakuna kundi lililodai mara moja kuhusika na shambulio hilo. Maafisa hao wamesema washambuliaji walikivamia kituo cha upekuzi na kisha kutoroka na gari lenye silaha lakini ndege ya kivita iliwafukuza katika eneo la jangwa na kufanikiwa kuwauwa washambuliaji watano.

Kwa miaka kadhaa Misri imekuwa ikipambana na wapiganaji wa kundi la itikadi kali lenye mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislam lenye makao yake kwenye jimbo la kaskazini la Sinai
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad