Simba Yasaka Mshambuliaji Hispania

Katika kuboresha kikosi chake kuelekea msimu ujao wa soka, klabu ya soka ya Simba imeelezwa kuwa ipo kwenye mawindo ya kupata sahihi ya mshambuliaji wa Tanzania anayekipiga Hispania Shabaan Chilunda.

Inadaiwa kuwa mwisho wa msimu huu wa 2018/19 Chilunda ambaye alikuwa anacheza Tenerife ya ligi daraja la kwanza Hispania, amevunja mkataba na timu hiyo.

Chilunda alikuwa akicheza kwa mkopo wa miaka miwili akitokea Azam FC, lakini anaelezwa kuvunja mtakaba wake baada ya msimu wa kwanza mambo kutomwendea vizuri ikiwemo kukosa nafasi ya uhakika ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.

Baada ya taarifa hizo za Chilunda kuvunja mkataba, Simba imeelezwa kuwa na nia ya kumsajili mshambuliaji huyo ambaye amewahi kuwa mfungaji bora wa klabu bingwa Afrika mashariki na kati.

Chilunda kwa sasa yupo kwenye kambi ya Taifa Stars inayojiandaa kwa ajili ya maandalizi ya fainali za AFCON 2019, zitakazofanyika nchini Misri kuanzia Juni 21 hadi Julai 19.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad