Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amelitangazia bunge hii leo kuwa ameiandikia tume ya uchaguzi ya nchi hiyo kuileleza kuwa jimbo la Singida Mashariki, lililokuwa likishikiliwa na Lissu kupitia chama kikuu cha upinzani Chadema lipo wazi.
Ndugai amesema kuwa sababu mbili kuu za kikatiba ndizo zimemfanya aiandikie tume ya uchaguzi kuhusiana na suala hilo.
Sababu ya kwanza ni kile alichokiita utoro wa Lissu bungeni. Japo inafahamika kuwa mwanasiasa huyo alilazimika kusafirishwa nje ya Tanzania kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiokulikana, kumekuwa na mjadala mkubwa juu ya kutokuwepo kwake bungeni kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Baada ya shambulizi dhidi yake Septemba 2017, Lissu alipelekwa Nairobi na kisha Ubelgiji kwa matibabu.
Bado yungali Ubelgiji akisema anaendelea na matibabu na hivi karibuni alitangaza kuwa atarejea Tanzania Septemba ili kushiriki katika chaguzi za serikali ya mitaa.
Lakini, wakati yungali ughaibuni, hasa katika kipindi cha miezi michache iliyopita amezuru Marekani, Ujerumani na Uingereza, kote huko, amehojiwa na vyombo vya habari za kutoa mihadhara kwenye vyuo vikuu juu ya hali ya haki za binaadamu Tanzania.
Hali hiyo iliibua hoja miongoni mwa wakosoaji wake kuwa tayari amepona na anastahili kurudi Tanzania.
Spika Ndugai mwezi Februari mwaka huu alikubali kufanyia kazi hoja ya kuzuia stahiki zake kama mshahara kwa madai hayo, na kusema kuwa hana taarifa rasmi juu ya alipo Lissu na hali yake ya kiafya, na amekuwa akimuona kwenye vyombo vya habari.
Lissu amekuwa nje ya Tanzania kwa matibabu toka Septemba 2017, amsema tarejea nyumbani atakaporuhusiwa na madaktari wake.
Hoja ya pili aliyoieleza Ndugai hii leo, ni kushindwa kwa Lissu kujaza na kupelekeka fomu ya tamko la mali na madeni ambayo viongozi wote wa umma ikiwemo wabunge wanatakiwa kujaza kwa mujibu wa sheria za Tanzania.
"Katiba yetu inasema, katika mazingira yote mawili (kutooneka bungeni bila taarifa rasmi, na kutowasilisha tamko la mali na madeni) ubunge wake unakoma na ataacha kiti chake, ndiyo lugha inayotumika na katiba…kwa hiyo unakuwa umejifuta mwenyewe ubunge, hujafukuzwa na mtu," amesema Spika Ndugai.
Lissu alikuwa miongoni mwa wanansiasa wa upinzani waliopendelea kumuita Magufuli kuwa 'Dikteta Uchwara' ama kwa lugha ya kingereza'Petty Dictator'.
Hatua hiyo imepokelewaje?
Muda mfupi uliopita chama cha upinzani cha CHADEMA kumeandika katia mtandao wake wa Twittet kuhusu hatua hiyo ya spika.
Ujumbe wa Twitter wa @ChademaTz
Tumemsikia Spika wa @bunge_tz Job Ndugai akitangaza kile alichodai kukoma ubunge wa Mwanasheria Mkuu wa Chama, Mbunge wa Jimbo la Singida Mash Mh @tundulissutz. Chama kitatoa kauli juu ya jambo hilo zito muda mfupi baadae. @bbcswahili @VOASwahili @dwnews @MwananchiNews @azamtvtz
Baada ya shambulio hilo, alikimbizwa Nairobi kwa matibabu kisha Brussels Ubelgiji toka mwezi Januari mwaka 2018.
Huko kote aliendelea kusisitiza kuwa serikali ya Magufuli ilikuwa na mkono kwenye shambulio dhidi yake.
Hata hivyo, katika miezi ya hivi karibuni Lissu ametoka Ubelgiji na kuzuru nchini Uingereza na kufanya mahojiano na runinga ya BBC, Kisha akazuru Ujerumani na kufanya mahojiano na runinga ya DW.
Kote huko, Lissu ambaye ni mbunge kupitia chama cha upinzani cha Chadema ameendelea kusisitiza kuwa serikali ya rais John Magufuli ilikuwa na mkono kwenye shambulio dhidi yake.
Pia amelishambulia Bunge chini Spika Job Ndugai kwa 'kumtelekeza' na kushindwa kulipia matibabu yake nje ya nchi.
Lissu pia amekuwa akilituhumu bunge chini ya Spika Job Ndugai kwa 'kumtelekeza' na kushindwa kulipia matibabu yake nje ya nchi.
Gharama za matibabu
Spika Ndugai aliliambia bunge kuwa si kweli kuwa chombo hicho kimtelekeza Lissu.
Ndugai alidai dai kuwa hadi mwishoni mwa Desemba 2018, Lissu alikuwa amelipwa Sh207.8 milioni pamoja na Sh43 milioni zilizotolewa kama mchango wa matibabu yake na wabunge wenziwe na kufanya jumla kuu ya fedha alizolipwa kuw Sh250milioni.
Hata hivyo, Lissu alimjibu Ndugai na kunukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema bunge la Tanzania halijawahi kutoa hata senti moja kugharamia matibabu yake.
Lissu amekiri kulipwa Sh43 milioni zilizotolewa na wabunge wenzake kama mchango wao na kwamba kiasi kingine alicholipwa kinachofanya jumla ya fedha hizo kufikia Sh250 ni mishahara na stahiki zake, lakini siyo gharama za matibabu.