Tabia za Wanawake Kuchukiana Bila Sababu..Nini Tatizo?



Ni hivi kwenye ofisi ninayofanya kazi tuko watumishi kama 15 hivi,kati ya hao wanawake tuko saa watano pamoja na ps,walobaki ni wanaume.

Basi kuna kipindi tulipewa zawadi ofisini,nami nilikuwepo miongoni mwa waliopata,tukiwa wanawake wawil tu tuliobahatika ,nikajipost kwenye group ya ofisini wanaume almost wote walikuwa happy na kunipongeza,ikaja kwa wanawake Sasa,mtu unakutana naye koridoni anakuuliza nimeona bana umepewa cheti,unamjibu ndio,anakwambia hongera huku ikiambatana na kicheko Cha kebehi na kejeli.

Ukija kwenye groups za wasap, comments wanazotoa wanaume kwetu wanawake si za kubeza,hata kama kukukosoa atakukosoa kistaarabu.Ila wanawake mtu atoa comments kama mna ugomvi,ama aweza comment neno la kukudhalilisha ilmradi usijisikie vizuri.Hadi wajiuliza ,tatizo nini?

Kuna wakati mwenzetu mmoja alikuwa mjamzito, jamaa mmoja wa ofisin akapiga naye picha akaipost kwa group,most of men walikuwa happy na walikuwa wanacomment positively,na matani ya hapa na pale,ila upande wa wanawake sasa wakatoa maneno ya kejeli na kuonyesha kutofurahia hilo jambo,as if wamechangia mume .Mwingine akaandika ,,ahhh mama kijaaa hongera bwana,then hehehehe halooo
,Like what the f@ck?

Hata kwenye ishu za deals ni mara chache,mwanamke akushirikishe hata kama una uwezo wa kulifanikisha,but kwa upande wa wanaume wako so smooth na washirikishaji wazuri.Tena wanawake hao wakigundua kuna kaishu unafatilia yuko radhi hata akuharibie kwa client,ili tu mkose wote.

Ishu ni nyingi,ila wanawake mostly hatupendani maofisini,Hatuko professional mostly,Tunasemana vibaya,tunaoneana wivu wa kijinga (siyo wa kimaendeleo),tunachafuana Wala hatusapotiani kwenye ishu positive.Nashindwa elewa tatizo ni nini.

So swali ni kwanini wanawake hatupendani?ni nature?Ni laana?Na suala la kutaka unnecessary competition na wanawake wengine sababu ni nini?

JF
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad