Taifa Stars na Harambee Stars ya Kenya Kuvaana Kesho Mjini Misri

Kesho Alhamisi timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itashuka dimbani kuchheza na Kenya 'Harambee Stars' katika michuano ya AFCON inayoendelea nchini Misri.

Kocha wa Kenya Sebastien Migne, tayari amezungumzia mchezo huo, "Mechi kati ya Harambee Stars ya Kenya na Taifa Stars ya Tanzania, itakuwa kama fainali kwetu. Tunatarajia kusajili ushindi wetu wa kwanza''.

Kwa upande wake kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike ameeleza kilichopelekea kupoteza mchezo wa awali dhidi ya Senegal kwa kusema kuwa tatizo la Afrika kila mtu anafahamu mpira.

"Kila mtu anaweza kukwambia mbinu na mifumo. Ni lazima tuseme ukweli, wachezaji wetu (Tanzania) wengi wanacheza ligi ya ndani, sasa huwezi kuwalinganisha na timu ambayo wengi wao wanacheza nje," amesema.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad