TAKUKURU yamshikilia Mhasibu Wizara ya Afya kwa ubadhirifu wa fedha

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), mkoani Kilimanjaro inamshikilia Mhasibu  wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa tuhuma za kufanya ubadhirifu wa  zaidi ya Sh. milioni 34 katika fedha za chanjo ya Rubella.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mjini Moshi, Kamanda wa TAKUKURU, mkoani hapo, Holle Makungu, amesema  taasisi hiyo inamshikilia Mhasibu huyo kutokana na kufanya makosa hayo kinyume na kifungu cha 22 na 28 vya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Amesema mhasibu huyo ambaye anajulikana kwa jina la Yahya Athuman, alimdanganya mwajiri wake na kufanya ubadhirifu wa fedha za umma zaidi ya Sh. milioni 34.2.

Aidha amesema Uchunguzi wa TAKUKURU unaonyesha kuwa mwaka 2014 wizara iliendesha zoezi la chanjo ya Rubella katika halmashauri mbalimbali ikiwemo halmashauri ya Moshi Vijijini na kwamba  wahasibu kutoka wizara hiyo walipewa jukumu la kusimamia fedha hizo na kufanya ubadhirifu huo.

“Sh. milioni 491.8 ziliwekwa kwenye akaunti na zilikuwa na maelekezo na Yahya alikabidhiwa ili asimamie matumizi katika Halmashauri za Manispaa ya Moshi, Moshi vijijini, Siha, Hai, Rombo, Mwanga na Same “amesema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad