TANZIA: Rais wa zamani Misri Mohammed Morsi aaga dunia mahakamani


Aliyekuwa rais wa Misri, Mohammed Morsi, aliyetimuliwa madarakani na jeshi mnamo 2013 ameaga dunia ghafla akiwa mahakamani, televisheni ya taifa inasema. 


Mahakama nchini Misri ilibatilisha hukumu ya kifo mnamo 2016 dhidi ya rais huyo aliyepinduliwa. 


Morsi alikumiwa kifo baada ya kulaumiwa kuhusika na kutoroka kwa wafungwa wengi wakati wa mapinduzi ya mwaka 2011 nchini humo. 


Alichaguliwa kuwa rais mwaka 2012 lakini akaondolewa katika mapinduzi ya jeshi mwaka mmoja baadaye, kufuatia maandamano makubwa ya kupinga utawala wake. 


Morsi ashahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa mashtaka yanayohusu ugaidi. 


Kwa muda wote, Morsi na wafuasi wake wamekuwa wakishikilia kukutu kuwa mashtaka dhidi yake yamechochewa na uhasma wa kisiasa baina yake na uongozi ulioko sasa. 


Morsi aliweka rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza kuchaguliwa katika uchaguzi wa haki na huru. 


Hata hivyo utawala wake ulikumbwa na wimbi la maandamano baada ya kujilimbikizia madaraka akiwa amehudumu kwa mwaka mmoja tu ya kuwa afisini. 


Tutakujuza zaidi kuhusu taarifa hii kadri tunavyoendelea kupokea maelezo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad